Kwa mujibu wa Shirika la Habari la AhlulBayt (a.s) -ABNA- utawala haramu wa Israel umetekeleza tena kitendo cha mauaji ya kulenga shabaha, na katika jinai yake ya karibuni kabisa, umemuua shahidi Haytham Ali Tabatabaei, mmoja wa makamanda mashuhuri wa Hizbullah nchini Lebanon. Mauaji haya ni sehemu ya sera ya muda mrefu ya kutekeleza mauaji ya kimfumo dhidi ya viongozi wa muqawama, sera ambayo imeendelea kwa miaka mingi.
Dkt. Ahmad Alwan, Mwenyekiti wa Chama cha Al-Wafa nchini Lebanon na mtafiti wa masuala ya kisiasa na kistratejia, katika mahojiano na ABNA alisema: Adui wa Kizayuni hudhani kwamba kwa kuwaua makamanda anaweza kuilemaza muqawama; lakini Hizbullah imejengwa juu ya misingi ya kazi ya pamoja, mfumo thabiti, na utaratibu wa maandalizi ya warithi wa kiuongozi. Kwa kila kamanda, kuna warithi walio tayari na waliofundishwa ipasavyo. Kwa hiyo, mauaji haya hayajawahi kudhoofisha irada ya muqawama, bali yamezidi kuimarisha azma yake ya kuendelea na njia yake.
Lengo halisi la utawala wa Kizayuni katika mauaji haya
Mtaalamu huyu kutoka Lebanon alisisitiza kuwa: Utawala wa Kizayuni kupitia mauaji haya na uvamizi unaoendelea unataka kuidhoofisha kipindi cha urais wa Lebanon na kuonesha kana kwamba Lebanon haitimizi wajibu wake wa kimataifa ili kujenga kisingizio cha kuendeleza uvamizi, kuleta machafuko, na hata kuhalalisha uingiliaji wa kijeshi wa kiwango kikubwa zaidi ndani ya Lebanon. Kwa hakika, lengo la mwisho la utawala huu ni kutekeleza ndoto yake ya upanuzi wa “Israel Kubwa” na kuangamiza kabisa muqawama katika eneo hili.
Athari za mauaji haya katika mizani ya kuzuia uvamizi
Dkt. Alwan alisisitiza kuwa mauaji haya hayataleta dosari yoyote katika mizani ya kistratejia ya kuzuia uvamizi. Muundo wa muqawama umetengenezwa kwa namna ambayo kila shahidi hubadilishwa na mrithi mwenye uwezo wa kiusalama na kijeshi katika kiwango kilekile. Akaongeza: Katika dunia ya leo, dhana kama vile “jamii ya kimataifa” na “haki za binadamu” kimsingi zimepoteza maana yao; mifumo ya sheria za kimataifa imetekwa na Marekani na Uzayuni, hivyo hakuna wa kuwanusuru watu waliodhulumiwa wa Lebanon.
Jibu la Muqawama: Lugha ya nguvu na moto
Mwenyekiti wa Chama cha Al-Wafa alisema: Tangu kutekelezwa kwa Azimio la 1701 na kusimamishwa kwa mapigano, muqawama ndiyo iliyoliheshimu, ilhali utawala wa Kizayuni umeuvunja zaidi ya mara elfu tano. Muqawama ilianza kwa kujaribu njia ya diplomasia, lakini iliposhindikana, ikaahirisha jibu lake hadi wakati na njia mwafaka. Lugha bora ya kuwakabili Wazayuni ni lugha ya nguvu na moto, na Hizbullah yenyewe ndiyo itakayochagua wakati, mahali na uzito wa jibu hilo.
Wajibu wa serikali ya Lebanon na hatari kubwa ya kuinyang’anya silaha muqawama
Dkt. Alwan alisema: Serikali ya Lebanon, kutokana na mipaka ya diplomasia na kutokuwepo kwa uimarishaji wa kweli wa jeshi (kwa sababu ya vizuizi vya Marekani), kimsingi haiwezi kuilinda nchi kijeshi. Pendekezo la kuinyang’anya silaha muqawama ni kosa kubwa la kistratejia. Badala yake, serikali inatakiwa kuilazimisha Israel kuondoka kabisa katika ardhi ya Lebanon, kuwaachilia wafungwa, na kusitisha uvamizi wake. Rais wa Lebanon anajaribu kuliepusha taifa kuingia vitani, lakini utawala wa Kizayuni haujawahi kutaka amani.
Your Comment